Serikali wilayani kahama yatatua chamgamoto ya madawati mashuleni

Katika kukabiliana na upungufu wa madawati katika shule ya Msingi Kangeme iliyopo halmashauri ya Ushetu, serikali wilayani Kahama mkoani Shinyanga imeanza mkakati wa kupeleka madawati 120 katika shule hiyo ili kusaidia kukabiliana na changamoto ya madawati katika shule hiyo.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa wilaya hiyo ANARINGI MACHA wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Ulowa kwenye mkutano wa kujadili namna ya kukabiliana na upungufu wa  vyumba vya madarasa  na madawati katika  shule ya Msingi Kangeme.

Amesema  madawati hayo yatakabidhiwa  feburia 10 mwaka huu huku akiwataka wananchi  kutambua kuwa ni wajibu wao kushiriki kuchangia miradi ya maendeleo ikwamo  ujenzi wa vyumba vya madarasa  na miundombinu mingine katika shule za misingi na sekondari.

Hata hivyo baadhi ya Wananchi wamesema kuwa wapo tayari kushiriki katika miradi ya maendeleo ikiwamo ya elimu na kuwaomba viongozi ndio wawe chachu ya kuwahamasisha wananchi waweze kuchangia kikamilifu.

Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Kangeme LAURIAN samesema wanaupungufu wa vyumba 33 vya madarasa na madawati  416, ili kutosheleza wanafunzi  2096 waliopo huku akisema kuwa madawati hayo yatasaidia katika vyumba vitatu vya madarasa ambavyo havikuwa kabisa na madawati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *