Serikali wilayani Kahama mkoni Shinyanga imeshauriwa kuungana na Mafundi  nguo  ili kusaidiana kuzalisha  barakao (Mask)

Serikali wilayani Kahama mkoni Shinyanga imeshauriwa kuungana na Mafundi  nguo  ili kusaidiana kuzalisha  barakao (Mask)  zitakazoweza kutumika bure kwa  makundi na wananchi wenye uhitaji katika kukabiliana na janga  la Corona Nchini.

Hayo yamesemwa leo mjini Kahama na Mwenyekiti wa umoja wa washona Nguo kata ya Kagongwa  Wilayani Kahama, MANYASA JOHN wakati wa kukabidhi msaada wa Baraka 200 kwa mkuu wa wilaya ya Kahama ANAMRINGI MACHA ili zigawiwe kwa makundi yenye uhitaji ikiwamo  kwenye  vituo vya watoto yatima.

Amesema  kutokana na kupanda kwa gharama ya mahitaji yanayotumika kutengengeneza barakoa  ni vema serikali ikatia mkoani wake ili waweze kufanikisha  azma ya serikali ya kuendelea kupambana na ugonjwa wa Covid 19 kwa wananchi kuvaa barakoa kwa gharama nafuu.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kahama ANAMRINGI MACHA amesema kuwa serikali wilayani humo itaanza kuwatumia mafundi  nguo katika kuzalisha barakoa kwa wingi na kwamba amepongeza hatua ambayo imefikiwa na umoja huo na kuahidi kuuelekeza msaada huo katika maeneo yenye uhitaji zaidi.

Umoja wa washona nguo Kata ya Kagongwa umezalisha  barakoa  zaidi ya 520 zenye thamani ya Shilingi zaidi ya shilingi laki tano ambapo pia wamekusida kwenda kugawa katika kituo cha kulelea watoto yatima  cha Buhangija  katika manispaa ya Shinyanga ambapo pia watagawa na vifaa kinga vingine kama  vile vitakasa mkono.

NDALIKE SONDA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *