Serikali wilayani kahama kuyashikilia magari ya wachimbaji wadogo

Serikali wilayani Kahama mkoani Shinyanga imesema itayashikilia magari yote ya wachimbaji wadogo wa dhahabu ambao wanakaidi agizo la serikali la kusimamisha uchimbaji wa dhahabu katika eneo la shule ya  Msingi Mwabomba kata ya Idahina halmashauri ya Ushetu.

Hayo yamesemwa leo mjini Kahama  na Mkuu wa wilaya hiyo, ANAMRINGI MACHA wakati wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama Cha Mapinduzi Ccm kwa muda wa miaka minne ya serikali ya  awamu ya tano katika wilaya ya Kahama.

Amesema licha ya serikali kupiga marufuku uchimbaji katika eneo la shule hiyo, baadhi ya wachimbaji wanaendelea na shughuli hiyo huku magari ya baadhi ya viongozi ambao wanashinikiza uchimbaji yamekuwa yakionekana eneo hilo.

February 12, mwaka huu, MACHA alitembelea eneo hilo  na kujionea uvamizi  huo na kuagiza uchimbaji katika eneo la shule  usimame na kwamba waendelee kuchimba nje ya mipaka ya shule ambapo hadi kufikia februari 17, mwaka huu walipaswa wawe wameondoka.

Mwenyekiti wa Ccm, wilayani Kahama THOMAS MYONGA ameipongeza serikali kwa utekelezaji mzuri wa ilani ya Chama hicho tawala miaka minne ndani ya serikali ya awamu ya tano ya Dokta JOHN MAGUFULI huku akielekeza  baadhi ya Changamoto  ambazo bado hazijatatuliwa zifanyiwe kazi kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka  2020.

 

Uvamizi wa eneo la shule Kwaajili ya uchimbaji ulianza tangu February mosi mwaka huu ambapo Idadi ya wachimbaji na wajasiriamali wengine walikuwa wanazidi kuongezeka licha ya marufuku ya serikali.

 

Katika hatua nyingine MACHA amesema katika Sera ya serikali  kuwakopesha Vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, kupitia asilimia 10 inayotengwa na halmashauri ipo changamoto ya   urejeshaji wa fedha kwa vikundi vya vijana ikilinganishwa na  vikundi vya wanawake ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika mikopo hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *