Serikali wilayani Kahama mkoani Shinyanga imesema itaanza kuwachukulia hatua za kisheria wananachi watakaoshindwa kusafisha mitaro inayopitisha maji katika barabara zote za mitaa kwa kuwa uchufu unaorundikana unasabanisha kuharibu miundombinu ya barabara.
Kauli hiyo imetolewa Jana na mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha wakati akikagua mitaro iliyohaririwa kwa mvua, katika mtaa wa Mayila mjini Kahama na kusema kuwa ni wajibu wa kila mwenye nyumba kusafisha mitaro ikiwamo kutoa mchsnga na udongi kwenye mitaro hiyo.
Amesema serikali haitasita kuchukua hatua ikiwamo kufunga vibanda by biashara kwa wanchi ambao watashindwa kutekeleza na kwamba viongozi wa serikali ya mtaa wasimamie Jambo Hilo.
Baadhi ya wananchi waliozungumza wamesema wamelipokea agizo la serikali ingawa wanaomba mitaro injengwe kila upande wa barabara ili kumudu Kasi ya kuyapokea maji yanayopita katika barabara za mitaa.
Barabara nyingi za mitaa mjini Kahama zimeharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, huku mitaro iliyongengwa katika baadhi ya barabara umeharibika kutokana na kukithiri kwa takataka, mchanga na udongo Hali inayosababisha maji kupita kwenye baraba na kusababisha kuharibika.