Serikali Wilayani Kahama imewaomba wadau kuchangia vifaa kinga na vifaa tiba kukabiliana na corona

Serikali wilayani Kahama mkoani Shinyanga imewaomba wadau mbalimbali kuendelea kusaidia vifaa vinavyosaidia kujikinga na janga la Corona ili viweze kusaidia wananchi hasa kwenye sehemu zenye mikusanyiko kama vile Sokoni, Hospitalini na gulioni.

Wito huo Umetolewa  mjini Kahama na Mkuu wa wilaya hiyo ANAMRINGI MACHA wakati akipokea  msaada wa mapipa 15 yalitotolewa na Mamlaka ya Maji ya Kahama-Shinyanga (KASHIWASA) kwaajili ya kununawia mikono wananchi katika kipindi hiki cha janga la Corona.

Amesema bado kunauhitaji mkubwa wa vifaa kama, sabuni, na vitakasa mikono katika maeneo yenye mwingiliano mkubwa wa watu, na kwamba Msaada walioupa utatumika katika maeneo ya huduma za umma katika halmashauri ya Mji wa Kahama, Ushetu na Msalala.

Naye Mkurugenzi wa KASHIWASA, JOSHUA  MAGEYEKWA amesema msaada huo wameutoa kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na janga la Covid 19 nchini.

MAGEYEKWA ameongeza kuwa KASHIWASA imetoa misaada hiyo pia katika wilaya zingine ambazo  inatoa huduma zake za Mji ikiwamo katika wilaya ya Misungwi na Kwimba mkoa wa Mwanza, Shinyanga na Kishapu kwa mkoa wa Shinyanga na Nzega,  Igunga na Uyuwi mkoani Tabora.

NDALIKE SONDA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *