SAMATTA KUIKOSA TUNISIA NOVEMBA 13

IMEELEZWA kuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachovaana na timu ya Taifa ya Tunisia Novemba 13.

Mbwana Samatta ambaye ni mshambuliaji jina lake lipo kwenye orodha ya wachezaji 27 walioitwa kuunda kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Kwa sasa Stars chini ya Kocha Mkuu, Ettiene Ndayiragije imeweka kambi nchini Uturuki ambapo nyota huyo anacheza nchini humo.

Habari zinaeleza kuwa Samatta hayupo kwenye mazoezi na timu ya Taifa ya Tanzania kwa kuwa ana matatizo ya kiafya na ameshauriwa na madaktari kutocheza ili arejee kwenye ubora wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *