Rwanda yawachukulia hatua mapadri kwa kukiuka muongozo wa kuzuia corona

Mamlaka nchini Rwanda imewachukulia hatua ya kinidhamu mapadri wa Kanisa Katoliki kwa kuendesha misa bila kuzingatia muongozo wa usalama wa kuzuia maambukizo ya virusi ya corona.
Parokia ya Kanisa Katoliki la Ruhengeri kaskazini mwa nchi hiyo, ambayo pia ni makazi ya mapadri hao inakabiliwa na tishio la kufungwa.

Mapadri hao, Emmanuel Ndagijimana na Felicien Nsengiyumva, wanasemekana hawakuzingatia idadi ya waumini waliotakiwa kuhudhuria misa kama iliyowekwa na serikali.

Polisi walikumbana “hali ya msongamano “katika kanisa na “kila mtu alikuwa katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi”, kwa mujibu wataarifa ya serikali.

“Tunayakumbusha madhehebu ya kidini hasa yale yaliyoruhusiwa kurejelea ibada kufuata muongozo uliowekwa wa usalama kama ilivyotolewa na mamlaka husika,” taarifa hiyo ilisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *