Ridhiwani Kikwete baada ya kusikia MO Dewji kajiuzulu Simba SC

Uamuzi wa muwekezaji wa Simba SC MO Dewji kujiuzuli uenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Simba SC umekuwa gumzo mtandaoni na kila mmoja anatoa mawazo na ushauri wake kuhusu uamuzi huo, mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ametumia ukurasa wake wa twitter kuandika ujumbe huu kwa MO Dewji kuhusiana na maamuzi hayo.

“Naheshimu sana Maamuzi ya Mtu lakini Brother sina hakika kama kafanya busara katika hili. Hela hazinunui Ushindi, ni haki yao kulipwa kwa kazi wanayoifanya. Please Brother, usifanye hasira. Huu ni Mpira tu na matokeo yako Matatu. Ninaamini utalifikiria tena uliloamua#MoDewji” >>>>Ridhiwani Kikwete
MO Dewji amefikia maamuzi hayo kutokana na kile kinachodaiwa na wengi timu hiyo kupoteza leo mchezo wa fainali ya Mapinduzi Cup 2020 dhidi ya Mtibwa Sugar kwa kufungwa goli 1-0, kutofanya vizuri katika mchezo wa January 4 2020 dhidi ya Yanga SC kwa kutoka sare ya 2-2 lakini kubwa ni kuishia round ya awali ya michuano ya CAF Champions League na kutolewa na UD Songo ya Msumbiji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *