RC Makonda kuhusu MO Dewji kujiuzulu Simba SC

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambaye pia ni shabiki mkubwa wa Simba SC, ametumia ukurasa wake wa instagram kuwaomba mashabiki wenzake wa Simba watulie, kuhusiana na taarifa ya twitter ya mwenyeki wao wa bodi MO Dewji kutangaza kujiuzulu nafasi yake kutokana na Simba SC kufungwa katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi 2020 kwa goli 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.

“Matokea ya Mpira huleta furaha na huzuni kwa wanaofungwa. Natoa pole Kwa team yangu ya Simba pamoja na Mashabiki wote na wanaoitakia mema SIMBA. Sina uhakika na kinachoendelea kwenye Ac ya MO kama ni @moodewji mwenyewe ameandika”>>>RC Makonda

“Nawaomba wanasimba tutulie tutapata ukweli muda si mrefu. Tusisahau kuwa Wapo watu pia wabaya hutumia mwanya huu kuvuruga Amani na utulivu wa Team zetu. Simba nguvu moja”>>>RC Makonda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *