Rais wa Uturuki ampokea Waziri Mkuu wa Libya

Baada ya mapokezi hayo, viongozi hao walifanya mkutano uliodumu saa moja, katika jumba la Vahdettin Köşkü lililoko mjini Istanbul.
Baadaye kulifanyika mkutano baina ya wajumbe wanaowalikisha serikali za pande zote mbili.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mawasiliano, viongozi hao walijadili uhusiano kati ya nchi mbili husika, na maendeleo ya kikanda.

Rais Erdoğan aliahidi kuwa Uturuki itaendelea kushikamana na kuweka ushirikiano kwa Libya, huku ikiendeleza juhudi zake za kuimarisha mahusiano na serikali ya maridhiano ya kitaifa inayotambulika kuwa halali.

Akibainisha kuridhishwa na hatua Umoja wa Mataifa kusajili mkataba wa makubaliano kuhusu utawala wa mpaka wa bahari Rais Erdoğan, alisisitiza kwamba Uturuki pia ipo tayari kuendelea kusimama bega kwa bega na Libya ili kuimarisha amani, utulivu, na ustawi wa nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *