Rais wa ukraine atangaza Watu wote 176 kwenye ndege wamefariki

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema hakuna aliyenusurika katika ajali iliyotokea leo asubuhi baada ya Ndege ya Ukraine ‘ Boeing-737’ kuanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Imam Khomeini, Iran na kwamba Watu wote 176 waliokuwemo ndani ya Ndege hiyo wamefariki.

“Nimesikitishwa na ajali hiyo na natuma salamu za pole kwa Ndugu na Marafiki wa abiria wote pamoja na wafanyakazi wa Ndege hiyo, Ukraine inachunguza mazingira yaliyosababisha ajali hiyo pamoja na vifo”  RAIS Ukraine

Abiria waliokuwemo kwenye Ndege hiyo ni Raia 82 kutoka Iran, 63 Canada, 11 Ukraine pamoja na wafanyakazi, Sweden 10, wanne ni Afghans, watatu British na watatu Wajerumani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *