Rais Putin ashuhudia makombora yenye uwezo wa kubeba silaha za nyuklia

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameshuhudia leo majaribio ya makombora yenye uwezo wa kubeba silaha za nyuklia ya Kinzhal na Kalibr katika jimbo lililochukuliwa na Urusi la Crimea, rasi katika bahari nyeusi iliyounganika na Ukraine bara.

Hatua ya Urusi kulichukua eneo hilo tangu mwaka 2014 kulizusha malalamiko mengi kimataifa. Shirika la habari la Urusi, TASS, limeripoti kuwa ndege mbili za kivita chapa MiG-31K zilifanya mazowezi ya kushambulia makombora hayo ya masafa marefu ya Kinzhal.

Ripoti hiyo imesema meli kadhaa za kijeshi ikiwa ni pamoja na meli ya kivita ya Admiral Grigorovich na nyambizi ya Kolpino zilifanya mazowezi zikifyatua makombora ya Kalibr.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *