Radio za kijamii zatakiwa kuyafikia makundi yote katika jamii ili kupata matokeo chanya.

Na William Bundala (Kijukuu cha Bibi K)

Mwanza

Radio za Kijamii nchini zimetakiwa kutafuta njia bora ya kuwasiliana na makundi mbalimbali katika jamii ili kujua uhitaji wao kwa lengo la kupata matokeo Chanya.

Wito huo umetolewa jana na mkufunzi kutoka Shirika la Elimu, Sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) Sebastian Okiki katika mafunzo ya Mwonekano na Mawasiliano ndani ya vyombo vya habari  yanayokutanisha Radio tano kutoka kanda ya ziwa.

Okiki amesema kuwa kuna makundi Mengi katika jamii yanayohitaji Radio kufikisha mahitaji yao lakini mambo mengi hayasikiki kutokana na radio nyingi kushindwa kuwafikia.

Ameongeza kuwa vipindi vya radio vinaweza kugawanyika na kuyafikia makundi mbalimbali kutokana na maudhui ya vipindi hivyo ili kuwezesha jamii kutoa maoni yao na radio kuyafikisha kwa watu wenye dhamana.

Naye mratibu wa Mafunzo hayo kutoka UNESCO Rosemary Mwalongo amezitaka radio za kijamii zinapoandika andiko mradi kuacha kubagua makundi ya kufanya nayo kazi kwani huwezi jua wafadhili wanataka kufanya kazi na makundi gani katika jamii inayozunguka radio yako.

Mafunzo ya Siku nne ya  Mwonekano na Mawasiliano katika radio kwa kanda ya ziwa Yameshirikisha Radio Kahama kutoka Shinyanga,Radio Kwizera kutoka Kagera,Radio Mazingira kutoka Mara,Radio Sengerama kutoka Mwanza na Radio Storm kutoka Geita.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *