Profesa Ibrahim Lipumba Aendelea Kunadi Sera Zake

Chama cha Wananchi CUF kimeahidi kuhakikisha kinaboresha miundombinu ya makao makuu ya nchi jijini Dodoma iwapo kitapata ridhaa ya kuongoza Serikali katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu.

Ahadi hiyo imetolewa na mgombea urais wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, Akijinadi katika alipokuwa akihutubia mkutano wake wa kampeni wilayani Chamwino, mkoani Dodoma.

Amesema ili wananchi wa Dodoma waweze kunufaika na kilimo na ufugaji wanahitaji kutafuta masoko kwa njia ya mtandao.

Profesa Lipumba akiwa ameambatana na mgombea mwenza, Hamida Abdalah Huweish, aligeukia ufugaji wa mbuzi akisema mifugo hiyo ni biashara nzuri ndani na nje ya nchi, lakini hakuna utaratibu unaowahakikishia wafugaji ufugaji bora.

Aidha amesema ili mbuzi waweze kuwa na soko ni lazima wafanyabiashara wajue kufanya biashara kupitia mitandao na kujenga utaratibu wa vijana kujielimisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *