Petrobena wawafikia wakulima wa Pamba Ushetu,Wawapa darasa kuhusu matumizi ya dawa ya Ruruka.

Wakulima wa pamba katika halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kufuata vipimo sahihi vya dawa ya kuulia wadudu wanaovamia zao hilo ili iweze kufanya kazi vizuri na kutoa matokeo chanya.

Wito huo umetolewa jana na bwana shamba wa kampuni ya Usambazaji wa pembejeo nchini Petrobena Emmanuel Kitosi wakati akitoa semina ya matumizi bora ya dawa mpya ya RURUKA ya kuuwa wadudu katika zao la pamba.

Kitosi amesema kuwa wakulima wengi wanashindwa kupata matokeo chanya pindi wanapotumia dawa za kuuwa wadudu kwakuwa hawazingatii vipimo vya kitaalamu pamoja kushindwa kuchanganya vyema dawa na maji.

Katika hatua nyingine Kitosi amesema kuwa dawa ya Ruruka inayosambazwa na Petrobena ina uwezo wa kuuwa wadudu kwa kutumia njia tatu ambazo ni kwa mdudu kula jani lenye dawa hiyo,Kwa kuvuta harufu na kugusa majani.

Nao baadhi ya wakulima wa zao la Pamba katika halmashauri ya Ushetu Daudi Charlse na Magreth Amocy  wameishukuru kampuni ya Petrobena kwa kuwafikia na kuwapa semina hiyo kuhusu matumizi sahihi ya dawa ya RURUKA kwani kampuni nyingi hazifiki mashambani na kutoa elimu hiyo.

Dawa mpya ya RURUKA ya kuuwa wadudu wanaoshambulia zao la Pamba inatolewa na Kampuni ya Suba Agro na inaujazo wa Gramu 150 kwa pakti moja na inasambazwa na kampuni ya Petrobena kwa wakulima wa Pamba katika Mikoa ya Kanda ya ziwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *