Panya Mtanzania aliyenusa Mabomu 39 atunukiwa Nishani ya Dhahabu.

Kuna hii ya kuifahamu leo September, 25, 2020 ambapo panya mkubwa alipewa mafunzo na Shirika lisilo la kiserikali- Apopo kutoka Ubelgiji lenye makao yake nchini Tanzania amepewa nishani ya dhahabu kutokana na uwezo wake wa kubaini mabomu ya kutegwa ardhini.

Panya huyu aliepewa jina la Magawa ameweza kunusa mabomu 39 na silaha 28 ambazo hazijalipuka katika maisha yake.

Shirika la Matibabu ya Wanyama la Uingereza lisilokuwa la kiserikali PDSA limemtuza medali ya dhahabu “kwa kujitolea kwake kuokoa maisha kupitia kazi yake ya kubaini mabomu hatari yaliyotegwa ardhini Cambodia”.

Inadhaniwa huenda kuna hadi mabomu Milioni sita ya kutegwa ardhini katika nchi hiyo ya kusini mashariki mwa bara Asia.

Nishani ya dhahabu ya PDSA, imeandikwa maneno “Kwa juhudi za wanyama au kujitolea kazini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *