OXFAM YATOA VIFAA KINGA KWA WATAALAMU WA AFYA MSALALA KAHAMA

Katika jitihada za kukabiliana na Ugonjwa  unaosababishwa na virusi vya Corona  katika Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama mkoani Shinyanga Shirika la OXFAM limetoa msaada wa vifaa kinga mbalimbali vya kukinga  na maambukizi kwa wataalamu wa afya vyenye thamani ya Shilingi Milioni 29 laki  nane na mia nane.

Akikabidhi vifaa hivyo leo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Simon Berege,Mratibu wa Miradi wa Shirika la OXFAM kanda ya Ziwa,Valentine Shibula amesema kuwa Msaada huo umetolewa kwa lengo la kuunga mkono jitihada za serikali katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Corona.

Amesema kuwa OXFAM kwa kutambua Umuhimu wa huduma zinazotolewa na wataalamu wa afya imeamua kutoa vifaa hivyo kwao ili kuwakinga na maambukizi ya Corona pindi wanapokwa wanawahudumia wagonjwa katika vituo mbalimbali vya afya  maalumu vilivyotengwa na serikali.

“vifaa tulivyowaletea leo ni pamoja na Barakoa za  (N95)240, Mavazi maalumu ya kujikinga na corona(PPE) Jezi 60 ,vidonge vya  kutakasa vifaa tiba vinavyotumika kwa wagonjwa kopo 12 na barakoa za kawaida  paketi 978 ambavyo vyote vimegaharimu zaidi ya shilingi milioni 29 vilivyonunuliwa katika bohari ya dawa (MSD),”amesema Shibula.

Akipokea vifaa hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Simon Berege amelipongeza shirika la OXFAM kwa kuiunga mkono serikali katika Mapambano dhidi ya COVID 19 na kuahidi kuwa vitatumika  ilivyoelekezwa katika kituo maalumu cha uangalizi wahisiwa wa Corona cha Bugarama.

“Niwatoe hofu wananchi katika Halmashauri ya Msalala tangu ugonjwa wa Corona Uripotiwe hapa nchini hapajawahi kutokea mtu yeyote anayeumwa ugonjwa huo na hadi hii leo hakuna mgonjwa yeyote katika kituo cha afya bugarama anayehisiwa kuwa na Corona,”amesema Berege.

Nae Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dk Ernest Chacha amesema kuwa kwa sasa wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi hususani katika maeneo yenye mikusanyiko kama vile minada na machimboni ili waendelee kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona.

“Tunaendelea kuwasihi wananchi waendelee kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Waataalamu wa afya ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa maji tiririka,kupaka vitakasa mikono na barakoa katika maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ili kuwakinga na virusi hivyo,”amesema Chacha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *