Ofisi nyingine ya Kata yachomwa moto Morogoro.

Ofisi ya Mtendaji wa kata ya Mlali wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro imechomwa moto usiku wa kuamkia leo na kuteketeza baadhi ya nyaraka za ofisi hiyo.

Kufuatia tukio hilo mkuu wa mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama mkoa wa Morogoro kuwatafuta na kuwakamata waliohusika na tukio hilo.

Katika tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na tayari watu watatu wameshakamatwa wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo.

Ikumbukwe usiku wa kuamkia jana Ofisi ya mtendaji wa Kata ya Soweto mjini Moshi imenusurika kuteketea kwa moto baada ya watu wasiojulikana kuchoma moto sehemu ya ofisi hiyo na kuteketza baadhi ya nyaraka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *