NECTA yatoa onyo kwa watakaovuruga mitihani

Watahiniwa milioni moja,elfu ishirini nne na mia saba wanatarajiwa kuanza mitihani ya kuhitimu Elimu ya msingi kuanzia kesho Oktoba 7 hadi 8, 2020 na watahiniwa 974,532 watafanya mitihani hiyo kwa lugha ya kuswahili huku watahiniwa  49,475 watafanya kwa lugha ya kingereza.

Akizungumza na vyombo vya habari Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Charles Msonde amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika ikiwemo kusambazwa kwa karatasi za mitihani, fomu maalum za ‘OMR’ za kujibia mitihani na nyaraka zote muhimu zinazohusika katika mtihani huo katika Halmashauri na Manispaa zote nchini.

“Baraza linatoa wito kwa wasimamizi wote walioteuliwa, kufanya kazi yao kwa uadilifu wa hali ya juu na wahakikishe wanalinda haki ya watahiniwa wenye mahitaji maalum” amesema Dkt. Msonde.

Ameongeza kuwa, Baraza linawataka wamiliki wa Shule kutambua kuwa shule zao ni vituo maalum vya mitihani na hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingilia majukumu ya wasimamizi wa mitihani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *