Ndege ya Tanzania iliyokamatwa Canada Kutua Nchini Kesho Jumamosi…Mapokezi Yake Ni Jijini Mwanza

Ndege aina ya Bombardier Q400 ya Tanzania iliyokamatwa nchini Canada inatarajiwa kuwasili nchini Disemba 14 mwa huu na itapokelewa jijini Mwanza.

Hii ni baada ya hapo jana kwenye Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa (NEC), Mwenyekiti CCM ambaye ni Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kusema ndege hiyo imeachiwa na itawasili nchini.

“Kwanza kwa taarifa tu Ndege yetu iliyokuwa imeshikwa Canada imeachiwa, mtatangaziwa tarehe ya kuipokea na mtaipokea hapa hapa Mwanza” alisema Rais Magufuli.

Ikumbukwe kuwa Novemba 23, 2019, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, alisema Ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400, imekamatwa nchini Canada.

Aliyesababisha ndege hiyo kushikiliwa ni yuleyule, Hermanus Stayn raia wa Afrika Kusini, aliyekuwa amefungua kesi na kusababisha ndege ya Tanzania aina ya Airbus A220-300 kushikiliwa nchini Afrika kusini, Agosti mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *