Namshangaa Spika akiwa bungeni yuko kiti cha pekeake anavaa barakoa- JPM

“Corona imekwisha ndio maana hata Mabarakoa hakuna hata leo tunaonana tu hapa kawaida, ndio maana nilikuwa namshangaa Spika Ndugai akiwa Bungeni yupo kiti chake peke yake lakini amelivaa hilo libarakoa mdomoni, Watanzania tumtangulize Mungu”-JPM

“Njia nyingine ambayo inaweza kutumika ni kuletewa vifaa vya corona vyenye corona, anapokuletea Mtu barakoa hujui ameitoa wapi kataa, mwambie kavae wewe na Mke wako na Watoto wako nyumbani, tutaumizwa”-JPM

“Ukitaka kuvaa barakoa kashone yako, mbona ni rahisi tu, barakoa mbona imekaa kama titi moja la Mtu mmoja hivi limekatwa upande mmoja, weka huku kama… aaah samahani Mh.Waziri nimesema hapa, nilikuwa nachomekea tu kidogo” -JPM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *