Mwanamke wa Marekani anaetakiwa kufariki kabla ya December 9

MAREKANI.

Lisa Montgomery, Mfungwa Mwanamke Kansas Marekani ambae anatakiwa awe amefariki kabla ya December 9 mwaka huu ikiwa ni hukumu ya kwanza ya kifo kutolewa kwa Mwanamke Nchini Marekani kwa miaka inayokaribia sabini.

Lisa amehukumiwa kunyongwa baada ya kupatikana na hatia ya kumnyonga Mwanamke Mamzito wa Missouri mwaka 2004 nchini Marekani na kisha kumchinja kwenye tumbo lake na kumtoa Mtoto aliyekuwa ndani kwenye ujauzito uliobebwa.

Marehemu Bobbie kushoto, Mume wake katikati na Mtoto wao.

Alimuua Mjamzito huyo (Bobbie Jo Stinnett) baada ya kuona ameweka tangazo kwenye mtandao akimuuza Mbwa wake hivyo Lisa aliwasiliana nae kama Mteja anaetaka kumnunua Mbwa lakini walipoonana Lisa alimuua Mwanamke huyo aliyekua Mjamzito wa miezi nane na kuondoka na Mtoto aliyekuwepo tumboni kurudi nae kwake akidai amejifungua yeye.

Iwapo hukumu hii ya Lisa itatekelezwa basi atakua ni Mwanamke wa kwanza kutekelezewa hukumu ya kunyongwa Nchini Marekani toka mwaka 1953, Hukumu yake ya kifo itatekelezwa kwa kumchoma sindano yenye sumu tarehe 8 December 2020  ambapo hii inafanyika ikiwa ni karibu mwaka mmoja toka utawala wa Rais Donald Trump kusema utaanza tena kutekeleza hukumu ya kifo Nchini humo.

Muonekano wa moja ya vyumba vinavyotumika kunyongea Watu.

Hii hapa chini ni orodha ya Watu waliokua wamepangwa kunyongwa Nchini Marekani kuanzia mwezi September mpaka December mwaka 2020 ambapo jina la Lisa ni la pili kwa Watu wa December ambapo akinyongwa hiyo December atakua Mtu wa tisa kunyongwa Marekani toka utekelezaji wa hukumu ya kifo urejeshwe mwezi July.

Wakili ambae amekua akimtetea Lisa amesema Mwanamke huyo amekubali makosa yake lakini amekua na tatizo la akili toka mdogo hivyo hukumu ya kifo haimstahili kwani akili yake ilivurugika kutokana na mateso ya Mama yake Mlevi, kubakwa na kundi la Wanaume pamoja na kufanyishwa biashara ya ngono.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *