Mwanamke Atuhumiwa Kumchinja Mwanae na Kumla Nyama Ludewa

Mwanamke mmoja anaejulikana kwa jina la Christina Mlelwa(38) mkazi wa Kijiji cha Mavanga kata ya Mavanga kitongoji Cha mji mwema wilayani Ludewa mkoa wa Njombe anashikilikiwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumchinja mwanae Joseph Gumbilo(4) mwenye ulemavu wa viungo na kumla nyama
Awali akizungumzia tukio hilo mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrew Tsere anasema mapema baada ya kufikishiwa taarifa za tukio hilo alilazimika kufika eneo la tukio na kumhoji mtuhumiwa ambaye alikiri kutekeleza mauaji ya mwanae na kisha kumkata viongo vyake  na kumla huku viungo vingine kuvitupa porini na chooni.
Tukio hilo linaleta mshituko kwa kamati ya ulinzi na usalama mkoa na kumsukuma mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka kufika katika kijiji hicho kuzungumza na wananchi na kisha kutoa agizo kwa wakuu wote wa  wilaya za mkoa huo kukamata kijiji kizima na kuweka lockup endapo watagoma kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuhusu matukio ya mauaji
Katika hatua nyingine Olesendeka ameliagiza jeshi la polisi kusaka ukweli wa tukio hilo haraka na wahusika kufikishwa mahakamani kama ambavyo katiba inalinda haki ya kuishi ya kila binadamu bila kujali ulemavu wake.
Katika mahojiano ya awali na  jeshi la polisi, mama huyo ambaye anaonekana kuwa na matatizo ya akili amekiri kuua na kukata vipande vipande na kumla nyama huku masalia mengine ikiwemo fuvu la kichwa na miguu akiyatupa porini hatua ambayo ililazimu kamati ya ulinzi kuvamia pori na kukuta vitu hivyo.
Lakini Mume wake bwana Daniel Gumbilo anasema mke wake alisha wahi kufanya jaribio kama hilo miaka ya nyuma kwa mototo wao mwingine anaesoma ambapo majirani walinusuru maisha ya mototo wao .
Nae kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa anasema jeshi linaendelea kuchunguza kwa kina zaidi kuhusiana na tukio hilo ili wahusika wapewe haki yao ya hukumu ya uovu wao.
Kwa upande wa mtendaji wa kijiji cha Mavanga Fadhiri Tajiri alisema ni kweli tukio hilo limetokea na kwamba taarifa zaidi anasubiri muongozo kutoka kwa viongozi wake.
“Ni kweli Hilo tukio lipo lakini viongozi wangu wamesema wapo njiani wanakuja nasubiri muongozo wa kutoka kwao”alisema Tajiri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *