Mwanajeshi feki alivyonaswa na viroba vya bangi, Kamanda asimulia

Mfanyabiashara Hussein Sadick Juma mkazi wa Kimara temboni jijini DSM anashikiliwa na jeshila pilisi mkoani Morogoro kwa tuhuma ya kusafirisha Dawa ya kulevya aina ya bangi viroba 15 vyenye uzito wa Kilogramu 237 huku akiwa amevalia nguo zinazofanana na za Jeshi la Wananchi wa Tanzania.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akisafirisha dawa hizo kwa kutumia gari binafsi aina ya Prado yenye namba za usajili T. 168 BWB huku akisindikizwa na Teresphori Hamisi (40) mkazi wa mgeta wialayani mvomero.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *