Mustafa Kassem: amekufa baada ya kufanya mgomo wa kula nchini Misri

Kassem mwenye umri wa miaka 54 dereva wa taxi New York, ambaye asili yake ni Misri, alikamatwa alipokuwa ameenda kutembelea nyumbani Misri 2013, alishutumiwa kwa madai ya upepelezi na kushiriki maandamano yanayopinga serikali.

Bwana Kaseem alikuwa akikanusha madai dhidi yake.

Aliacha kula chakula mwaka jana na kwa siku nne zilizopita hakuwa akinywa kinywaji chochote.

Mwanadiplomasia wa juu wa Marekani Mashariki ya Kati, David Schenker, alielezea kifo cha Kassem kuwa cha kusikitisha, na ambacho kingeepukika.

Kassem alikamatwa Agosti 2013 mjini Cairo na maafisa wa usalama waliomshutumu kuwa jasusi na kushiriki maandamano dhidi ya serikali ya rais Abdel Fattah al-Sisi.

Kassem alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani 2018.

Kassem ambaye alikuwa anatembelea familia yake Misri wakati huo – alikanusha shutuma za kushiriki maandamano ambazo zilisababisha vifo vya watu zaidi ya 800 pale vikosi vya usalama vilipofyatua risasi dhidi ya waandamanaji, kulingana na Shirika Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch.

Kassem alishtumu wanajeshi wa Misri kwa kuchukua pasipoti yake ya Marekani na kuipiga muhuri wakati wanamkamata.

Kassem alikataa kula mara kadhaa wakati anazuiliwa.

Shirika la Kimataifa linalolinda haki za wafugwa wanaosubiri kuhukumiwa la Pretrial Rights International ambali lilimwakilisha, limesema kwamba aliaga dunia kwasababu ya ugonjwa wa moyo.

“Alhamisi iliyopita, aliacha kunywa kiywaji chochote na muda mfupi baada ya hapo alipelekwa katika hospitali, na kuaga dunia ,” taarifa imesema hivyo.

Wizara ya mambo ya ndani imesema kuwa alipelekwa katika hospitali ya wafugwa kutibiwa kisukari.

“Hali yake iliendelea kudorora… na aliaga dunia Januari 13, taarifa imesema hivyo.

Bwana Schenker, mwanadiplomasia wa juu wa Marekani Mashariki ya Kati, amekitaja kifo cha Kassem kuwa cha masikitiko makubwa na kwamba kiliweza kuepukika, lakini hakusema iwapo kifo hicho kitakuwa na athari zozote kwa Misri – mshirika wa karibu wa Marekani.

Mwendesha mashtaka wa Misri ameagiza mwili wake ufanyiwe uchunguzi kubaini sababu za kifo chake, shirika la habari la Misri, Mena limesema.

“Mfungwa mwengine ambaye ameuawa gerezani, “ameandika kwenye mtandao wa Twitter mwanaharakati raia wa marekani mwenye asili ya Misri Aya Hijazi, ambaye alizuiliwa kwa karibia miaka mitatu nchini Misri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *