Msigwa, Lissu wawasilisha barua ya kutia nia ya kuwania Urais

Mbunge wa jimbo la Iringa Mjinikupitia chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA Peter Msigwa pamoja na Muheshimiwa Tundu Lissu wametangazwa kuwasilisha barua ya kutia niaya kuwania Uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanial

Kwa nyakati tofauti wamewasilisha barua hizo kwa katibu mkuu wa chama hicho ambapo Lissu anadaiwa kuongea na Watanzania muda wowote.

Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa na Mjumbe wa CC ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Peter Msigwa  amewasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, ya kutia nia ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mh Tundu Lissu amewasilisha barua rasmi ya kutia nia ya kuwa Mgombea Urais kupitia CHADEMA. Ndani ya siku 3 zijazo, Mh Lissu atazungumza na Watanzania na Jumuiya za Kimataifa juu ya nia yake hio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *