Msanii Vitali Maembe ajiunga ACT -Wazalendo na Kutangaza Nia ya Kugombea Ubunge

Mwanamuziki Vitalis Maembe amejiunga na Chama cha ACT-Wazalendo na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu

Maembe amejiunga na chama hicho leo Jumatatu tarehe 29 Juni 2020 na kukabidhiwa kadi na Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa chama hicho, makao makuu ya ACT-Wazalendo, Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Maembe amesema ACT-Wazalendo ni chama chenye sifa anazozihitaji kama vile yeye anavyojipambanua kwenye muziki wake.

Akimkabidhi kadi ya uanachama Jana jijini Dar es Salaam , Ado amemuhakikishia Maembe kuwa ACT Wazalendo litakuwa jukwaa sahihi kwake kuendeleza mapambano ya kudai haki.

Amesema, zaidi ya haki ataendelea kupinga rushwa na kupigania umoja wa Afrika kama ambavyo amekuwa akifanya siku zote kupitia sanaa.

Mbali na kuchukua kadi hiyo lakini pia Maembe aliyewahi kuimba nyimbo ya “Sumu ya teja”, “vuma” ametangaza nia ya kugombea Ubunge kwenye Jimbo la Bagamoyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *