Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji mstaafu Francis Mutungi Aionya CHADEMA

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji mstaafu Francis Mutungi amewaonya CHADEMA kutokana na alichokiita Uvunjifu wa Sheria kwa kuongeza beti la tatu kwenye wimbo wa Taifa.

Mutungi ametoa onyo hilo mara baada ya jana CHADEMA wakati wakiendelea na vikao vya kupitisha jina la  atakaye peperusha bendera ya Chama hicho katika nafasi ya Urais akisema hakutegemea kwa Chama kikongwe Kama CHADEMA kufanya kitendo hicho.

“Kitendo walichofanya sio cha kukaliwa kimya, kilichonisikitisha ni kitendo cha uvunjifu wa Sheria kwa makusudi, kitendo kilichofanyika na CHADEMA ni lile jambo la kuchukua Wimbo wa Taifa na kuongeza aya ya tatu na mbaya zaidi wanasema wanaongeza tuone kinachotokea” Mutungi

“Rais alionya Wanasiasa wasichokoze Vyombo vya dola, nawakumbusha hakuna Taasisi iliyo juu ya Sheria, kilichofanyika ni kama kunajisi wimbo wa Taifa” Mutungi

Amesema kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania na Zanzibar ni kosa huku akivikumbusha vyama vya siasa vyote vinavyoendesha michakato katika vyama vyao kukumbuka kwamba Sheria hazijakwenda likizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *