Moto wasababisha uharibifu kwenye mgodi wa dhahabu buzwagi

Ajali ya Moto  imetokea jana katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi wilayani Kahama mkoani Shinyanga kwenye  mtambo wa kuchenjulia dhahabu na Kusababisha uharibifu wa vifaa mbalimbali  vilivyokuwa katika eneo hilo.

Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji wilayani Kahama Inspekta DUMA MOHAMED akizungumza na waandishi wa habari amesema  ajali hiyo imetokea majira ya saa  11:45 asubuhi na kwamba chanzo cha awali ni  inaelezwa  ni joto.

Amesema kwa  bado haijajulikana thamani halisi ya vifaa  hivyo ingawa  vitu vyote  vimeharibika ikiwamo matanki ya mafuta ya petroli na disel pamoja na kemikali mbalimbali zinazotumika kuchenjulia dhahabu.

Akitoa maalezo kwa jeshi la zimamoto na uokoaji  msimamizi wa mitambo hiyo katika mgodi huo  KULWA MARUNGA amesema waliona moshi  ukitoka kwenye  tanki moja wapo la mafuta  baada ya  kuwasha mitambo hiyo katika chumba maalumu cha kuwashia mitambo hiyo.

Matukio ya ajali za moto katika  wilaya ya Kahama  yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara katika  makazi ya watu  na kwamba jeshi la zimamoto na uokoaji  limeitaka jamii na taasisi kuendelea kuchukua tahadhari ya majanga ya moto.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *