mlemavu wa miguu anufaika na msaada kutoka kwa kikundi cha akina mama kahama

Kikundi cha wakina mama NEW KAHAMA FRIEND GROUP kilichopo wilayani kahama mkoani shinyanga wamekabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa Mtoto mwenye umri wa miaka 11 mlemavu wa miguu anayeishi katika kijiji cha bukandu wilayani mbogwe Mkoani geita.
Akizungumza jana wakati wa kukabidhi msaada huo kiongozi wa kikundi hicho cha kina mama CATHERINE MEZA amesema kuwa wao kama kina mama wameguswa na changamoto ya ulemavu wa mtoto huyo kutokana na mazingira anayoishi .

MEZA amesema kuwa wametoa viti viwili vya magurudumu matatu, godoro moja, nguo pamoja na mahitaji mengine mbalimbali na pesa taslimu shilingi elfu 27 ambapo vitu hivyo vimegharimu zaidi ya shilling laki saba.

Kwa upande wake mtoto huyo ambae anajulika kwa jina la MAPESA MAYUNGA amewashukuru wakina mama hao kwa msaada huo walioutoa na kusema kuwa waendelee na moyo huo hata kwa watu wengine wenye mahitaji muhimu.

MAPESA MAYUNGA ni mtoto ambaye amezaliwa bila miguu na anaishi na bibi pamoja na baba yake baada ya kutelekezwa na mama yake na kuolewa na mwanaume mwinggine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *