Mke azika mwili wa mumewe mara mbili.

Mwanamke mmoja Afrika Kusini amelazimika kufanya mazishi ya mume wake mara mbili aliyekufa kwa ugonjwa wa Covid-19 baada ya kubainika kwamba mwili wake ulitambuliwa makosa.
“Walikataa kuniruhusu nione mwili wa mpendwa wangu katika chumba cha kuhifadhia maiti kwasababu ya kanuni za kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19. Sasa nimemzika mtu mwingine.”
Hayo ndio yalikuwa maneno ya kusikitisha ya mke wake baada ya kubainika kwamba mwili wa mume wake, 79, umechanganyika na wa mwingine.
Micheal Vukile Noda, kutoka Uitenhage, mashariki mwa Cape alianza kuonesha dalili za ugonjwa wa Covid-19 na hali yake ilipoanza kuzorota mke wake akatafuta matibabu Juni 16. Mara ya mwisho familia yake kumuona ni pale alipobebwa na gari la kubebea wagonjwa akipelekwa hospitali.
Kulingana na mke wa Vukile, Nomsa Noda, 69, alikuwa na mafua kwa muda wa wiki mbili.
“Alienda kumuona daktari lakini hakumaliza matibabu kwasababu alilazwa kabla ya kumaliza dawa,” anasema.
Hali yake ilibadilika na akapelekwa kitengo cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi, anasema.
Hospitali iliarifu familia kwamba amepata maambukizi ya mapafu.
Baadae alihamishwa hadi wadi ya wagonjwa wa kawaida na kuwa huko kwa wiki moja.
“Kwasababu hatukuruhusiwa kumtembelea, mara nyingi tulizungumza kwa simu. Lakini kadiri tulivyokuwa tunaendelea kuzungumza, alionekana kuwa dhaifu na mchovu sana hata kuongea ilikuwa shida. Ikafika kipindi ikawa hawezi hata kujibu simu zake unapompigia,” amesema Nomsa.
Nomsa aliendelea kuwasiliana na wauguzi kuhusu hali ya mgonjwa wake lakini kila wakati walikuwa wanamuarifu kwamba mume wake yuko salama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *