Mkapa aonya udini, ukabila na umaskini

Dar es Salaam.

Katika maisha ya Watanzania si rahisi kuona waziwazi masuala kama ya udini, ukabila na ukanda, lakini Benjamin Mkapa, ambaye ameliongoza Taifa hili kwa miaka kumi, anaona kuna dalili ya mambo hayo hatari kwa mshikamano wa nchi.

Pia anaonya kuhusu umaskini, akisema ni kitu kingine kinachoweza kuiingiza nchi katika machafuko iwapo hakitashughulikiwa.

Tanzania, ambayo ina takriban makabila 120 na dini kubwa mbili, ni moja kati ya nchi chache barani Afrika ambazo hazijatumbukia katika migogoro inayotokana mambo hayo, Kiswahili kikihusishwa na mafanikio hayo.

Lakini katika kitabu cha “My Life, My Purpose (Maisha yangu, Kusudi Langu)”, Mkapa anaonyesha wasiwasi wa mambo hayo kukua na kuonya kuwa yakiendelea yanaweza kuvuruga amani ya nchi.

Mkapa anasema tangu kuasisiwa kwa Taifa la Tanzania, kumejengwa misingi imara ya umoja ambayo imekuwa mfano kwa mataifa mengine.

Bila ya kuweka bayana, Mkapa anasema katika miaka ya karibuni kumekuwa na viashiria vya kuibuka kwa udini, ukabila na ukanda.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *