Mkandarasi wa Umeme wa REA Ushetu Kahama,Atajwa na madiwani kuwauzia wananchi nguzo za umeme.

Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga limeagiza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa baadhi ya wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme (REA) ambao wanawatoza wananchi fedha ili kulipia gharama za nguzo na mita kinyume na maagizo ya serikali.

Wakizungumza katika kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo, Tabu katoto  diwani wa kata ya Igunda na Paulo Sai Golani diwani wa kata ya Kisuke wamesema wananchi wamekuwa wakitozwa fedha na baadhi ya watumishi wa kampuni ya ANGELIQUE INTERNATIONAL.CO.L.T.D ambayo inatekeleza Mradi wa REA katika vijiji 54 katika halmashauri hiyo.

Juma Kimisha ni Mwenyekiti wa Halmashauri amesema kitendo hicho kipaswa kupingwa kwa nguvu zote kwani si maelekezo ya serikali na wananchi wengi wameshindwa kupata huduma hiyo kutokana na urasimu uliopo katika miradi ya REA

Akijibu Malalamiko ya Madiwani hao Afisa Masoko wa shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutoka Makao makuu Musa Chowo amemtaka meneja wa TANESCO  wilaya ya Kahama Mhandisi King Fokanya kuhakikisha anawasimamia wakandarasi hao ambao wamebainika kuwaibia wananchi.

kampuni ya ANGELIQUE INTERNATIONAL.CO.L.T.D inayotekeleza mradi huo mpaka sasa imeweka umeme katika vijiji 14 kati ya 54 vya halmashauri ya Ushetu kandarasi ambayo imedumu kwa miaka miwili ambayo kwa sasa muda wake umeshaisha na hajakamilisha mradi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *