Michuano ya Kahama Fm Bonanza 2019,Yatajwa kuongeza kipato cha Mama lishe.

Na Ndalike Sonda,Kahama

Baadhi ya  wajasiriamali  katika mji wa Kahama mkoani Shinyanga  wamesema, kwa kiasi kikubwa   uchumi wao umeimarika kutokana na kupata fursa ya kuuza bidhaa mbalimbali ikiwamo vinywaji na chakula kwenye mechi za bonanza la Kahama fm 2019 lililofikia tamati  novemba 10, mwaka huu.

Wakizungumza  leo kwenye kipindi cha raha ya Leo cha Kahama fm, wajasiriamali hao wameipongeza Kahama fm, kwa kuandaa mashindano hayo ambayo yamewasaidia kukuza mitaji yao.

Kwa upande wake mratibu wa Mashindano hayo mwaka 2019, SEBASTIAN MASHINJI KOMAA amewapongeza wadau wote kwa kuyaunga mkono mashindano  hayo na kwamba watazidi kuyaboresha ili kila mwananchi aweze kunufaika nayo kwa njia mbalimbali.

Mashindano  ya bonanza la Kahama fm 2019 yamefanyika kwa karibu miezi minne jambo ambalo wajasiriamali hasa wa vinywaji, matunda na chakula wamejivunia  kwa kufanya biashara kwa muda mrefu katika mashindano hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *