MICHEZO Man United yamsajili Alex Telles

Club ya Man United imemsajili beki Alex Telles kutokea FC Porto ya Ureno kwa mkataba wa miaka minne.

Man United wamelipa euro milioni 15 kuhakikisha beki huyo wa kushoto anatua katika Man United baada ya dau hilo kutoka.

Hata hivyo leo ikiwa ndio siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili, Man United wamedaiwa kupotezea mpango wa kumsajili Ousmane Dembele kutokea FC Barcelona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *