Mhadhiri UDOM aanzisha Ushirika wa aina yake Tanzania,Lengo kuwafikia watu Milioni 20 ndani ya Miaka mitano

Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Dodoma aanzisha ushirika wa aina yake nchini Tanzania.

Ushirika huu ni tofauti na ushirika wa fedha yaani SACCOSS na ushirika wa mazao yaani AMCOS ambao umezoeleka katika fani ya ushirika.

Ushirika huu mpya ni ushirika wa Huduma ambao lengo lao ni kutoa huduma ya mawasiliano ya gharama nafuu na kusaidia ushirika uliopo kwenda digitali.

Akisema hayo, Mhadhiri Msaidizi huyo wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Mwl. Matogoro Jabhera amesema lengo lake ni kuwafikishia huduma ya Mtandao watu Mil. 20 ndani ya kipindi cha miaka mitano.

Huu ni mwendelezo wa jitihada zake za kutumia teknolojia ya mawimbi ya televisheni yaani “television white space” kwa ajili ya huduma ya mtandao.

Matogoro amesema, huu ni ushirika maalumu kwa ajili ya vijana na ushirika huu utatoa fursa za ajira kwa vijana wetu na kwa wananchi wote bila kujali viwango vya elimu zao wala fani zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *