Mganga wa kienyeji mkoani kigoma amehukumiwa kifungo cha maisha

Mahakama ya Wilaya ya Kigoma imemuhukumu Mganga wa Kienyeji, Venance Edward kwenda jela kifungo cha maisha baada ya kumkuta na hatia ya kubaka mtoto mwenye umri wa miaka 8.

Kesi hiyo namba 95 ya mwaka 2019 inayomkabili Venance Edward ambaye ni Mganga wa Kienyeji, kosa la kubaka alilolifanya katika eneo la Kasoko Ujiji  mnamo April 23, 2019, wakati mtoto huyo akipatiwa matibabu nyumbani kwake kinyume na kifungu cha 130 nakifungu kidogo cha 1 (E).

Awali Mashahidi wanne akiwemo Mtoto, Mama, Daktari na Mpelelezi wa Polisi uliwasilishwa mahakamani hapo kuhusiana na tukio hilo, ambapo ushahidi wa Daktari ulibainisha mtoto huyo kuwa alibakwa huku mshtakiwa akijitetea kutohusika na kitendo hicho.

Kwaupande wake Wakili wa Serikali, Raymond Kimbe aliomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa kama sheria inavyosema, ili iwe fundisho kwa watu wengine huku Mshtakiwa akijitetea kuwa Mahakama impunguzie adhabu kwani ni kosa lake la kwanza.

Baada ya Hakimu anayesikiliza kesi hiyo  Kitalo Mwakitalu kujilidhisha na ushahidi wa mlalamikaji pasina kuacha shaka akamuhukumu kwenda jela maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *