Matiko ajinadi kwa kutoa elimu ya mpiga kura

Mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA),Esther Matiko amewataka wapiga kura wenye sifa ya kupiga kujitokeza kwa wingi siku ya 10,28,2020.,ambayo ilipangwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi kuwa siku ya kupiga kura.

Matiko alisema jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyikia viwanja vya kata ya Turwa Rebu Senta ambapo aliwataka wapiga kura kujitokeza kwa wingi na kwenda kuwachagua viongozi wenye sifa ya kuwatumikia.

Matiko aliongeza kusema kuwa ndani ya miaka yake mitano kama mwanamke mbunge pekee jimbop la Tarime mjini ameleta maendeleo ndani ya halmashauri ya Tarime kwa kutumiafedha za mfuko wa jimbo pamoja na pesa yake ya mfukoni mwake huku akiwasemea watanzania kwa ujumla matatizo mbalimbali.ndani ya Bunge.

“Niseme wakati nikiwa mbunge nimeleta maendeleo ambapo wanaopinga ni vipofiu hawaoni hata ukufanyaje hawataona cha msingi wapiga kura wenzangu siku ya mwezi wa 10,28 mwaka huu nendeni kanipe kura zote za ndio ili niendeleze matakwa ya maendeleo ambapo nitahakikisha jimbo letu linapata maji,matibabu bora,miundombinu ya barabara na elimu bora kwa vijana wetu”alisema Matiko.

Pia mgombea huyo aliongeza kusema kuwa akichaguliwa atahakikisha ahadi zote anazitimiza kama alivyoahidi wakati akiomba kura.

Naye mgombea ubunge viti maalumu CHADEMA,Tekra Johanes aliwataka wapiga kura kutofanya kosa na waende kuwachagua viongozi wa Chadema kwasababu CCM imewatesa wananchi kwa mda mrefu na kuwa tangu uhuru bado wanaendelea kutoa ahadi.

Johanes aliwataka wapiga kura hususani vijana kuwa watulivu pale ambao uchaguzi utakuwa wa uhuru na haki isipokuwa watakapoona haki yao ikiporwa wataenda kuidai na kuitetea hadi dakika za mwisho.

Pamba Chacha ambaye ni mgombea udiwani kata ya Sabasaba ambae jina lake liliwekewa pingamizi aliomba wapiga kura kujitokeza kwa wingi siku hiyo nahata kama jina lake halitakuwepo katika baroti ya kupiga kura wawachague viongozi wa Chadema nawasifanye kosa la kuwachagua wagombea wa CCM.

Pamba alitupia lawama mkurugenzi wa halmashauri ya Tarime mjini kuwa amekuwa kikwazo cha pingamizi alilowekewa na kuendelea kuwasema yeye na Bashiri Selemeni kuwa wanamtishia kitu ambacho sikweli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *