Marekani yapitisha mswada wa kichocheo cha uchumi

Baraza la Wawakilishi nchini Marekani limepitisha mswada mpya wa kichocheo cha uchumi wa dola bilioni 483 wakati kiwango cha ukosefu wa ajira kutokana virusi vya corona kikipanda na makampuni yakihitaji msaada zaidi.

Mswada huo tayari ulikuwa umeidhinishwa na Baraza la Seneti, na Rais Donald Trump ameashiria kwamba atausaini haraka iwezekanavyo kuwa sheria.

Mswada huo ulikuja wakati wafanyakazi wengine wa Marekani milioni 4.4 wakiwasilisha maombi mapya ya kulipwa mafao ya ukosefu wa ajira, na kufikisha jumla ya watu milioni 26.4 tangu katikati ya Machi.

Karibu watu 50,000 wamefariki dunia Marekani kutokana na virusi vya corona, baada ya watu 3,176 kufariki dunia jana.

Idadi ya walioambukizwa ni 866,646 lakini kutokana na ukosefu wa vipimo, kamili huenda iko juu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *