Marekani yaishutumu Syria kwa kuchelewesha katiba kabla ya uchaguzi

Marekani na washirika kadhaa wa magharibi wameituhumu serikali ya Syria kwa kuchelewesha makusudi mchakato wa kuandika katiba mpya ili kuchelewesha muda hadi uchaguzi wa rais wa 2021, na kuepuka upigaji kura chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa kama ilivyoitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Naibu balozi wa Marekani Richard Mills amelihimiza Baraza la Usalama kufanya kila linalowezekana kuizuia serikali ya Bashar al-Assad kuyazuia makubaliano kuhusu katiba mpya katika mwaka wa 2020.

Azimio la Baraza la Usalama lililopitishwa Desemba 2015 iliidhinisha kwa kauli moja mpango wa kufikia amani nchini Syria ambao ulifikiwa jijini Geneva mnamo Juni 30 2012 na wawakilishi wa Umoja wa Mataufa, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Umoja wa Ulaya, Uturuki na wanachama wote watano wa kudumu katika Baraza la Usalama – Marekani, China, Urusi, Ufaransa na Uingereza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *