Makubaliano hayo yatatiwa saini mbele ya wasimamizi wa kimataifa baada ya mazungumzo ya muda mrefu kati ya wajumbe wa Umoja wa Falme za kiarabu,Taliban na Marekani.
Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid pia amefahamisha kwamba Marekani na Taliban watafanya mipango juu ya kubadilishana wafungwa wa kivita.
Mkataba kati ya Marekanai na Taliban utatiwa saini kutegemea na hatua zitakazochukuliwa ili kupunguza mapigano nchini
Afghanistan kote kwa kiwango kikubwa. Mkataba huo utatoa fursa ya kuleta amani baada ya miaka mingi ya vita na uwepo wa majeshi ya Marekani tangu mwaka 2001.
Katibu Mkuu wa mfungamano wa kijeshi wa NATO Jens Stoltenberg kwenye taarifa yake amesifu mkataba huo kuwa utafungua njia ya kuleta amani ya kudumu.
Amesema hatua hiyo inaweza kufungua njia ya mazungumzo kati ya Waafghanistan na hatimae kuhakikisha kuwa nchi hiyo sio tena mahala salama kwa magaidi.