Marekani iko ‘tayari kufanya mazungumzo’ na Tehran

Katika waraka wake kwa Umoja wa Mataifa, Marekani ilijitetea kuwa ilimuua jenerali wa jeshi la Iran Qasem Soleimani kama hatua ya kujilinda

Iran ilijibu hatua hiyo kwa kushambulia kwa makombora kambi ya majeshi ya Marekani nchini Iraq japo hakuna mtu aliyejeruhiwa.

Jenerali Soleimani ilichukuliwa kuwa afisa wa pili wa ngazi ya juu nchini Iran.

Kama mkuu wa kikosi maalum cha Quds Force, katika jeshi la ulinzi la Revolutionary Guards’ alilikuwa mtekelezaji wasera za Iran katika eneo la mashariki ya kati.

Kiongozi mkuu wa kidini wa Iran Ayatollah Khamenei amesema shambulio hilo lilikuwa “kofi la usoni” kwa Marekani na kutoa wito kwa nchi hiyo kuondoka mashariki ya kati.

Shambulio dhidi ya Soleimani pia liliwaua wanachama wa kundi la waasi wanaounga mkono Iran ambao pia wamesema watalipiza kisasi.

Hatahivyo, makamu wa rais wa Marekani Mike Pence ameimbia kituo cha habari cha CBS kwamba “ujaususi” unaashiria kuwa Iran imewaambia waaasi hao ambao ni washirika wake wasishambulie ngome zozote za Marekani.

“Tunapokea taarifa za ujasusi za kutia moyo kwamba Iran inatuma ujumbe kwa baadhi ya waasi kutoshambulia ngome za Marekani ama raia, na tunatarajia wataendelea kutoa ujumbe huo,” Bw Pence aliambia kituo hicho.

Bunge la wawakili baadae leo Alhamisi linajiandaa kudhibiti uwezo wa rais Donald Trump kuanziwa vita dhidi ya Iran bila idhi maalum kutoka kwa Congress.

Katika barua iliyotumwa kwa baraza lausalama la Umoja wa mataifa, balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa Kelly Craft alisema Marekani iki tayari kufanya mazungumzo na Iran “kwa lengo la kuzuia hatari itakayoathiti amani na usalama wa kimataifa”.

Mauaji wa Soleimani yalistahili, barua hiyo ilisema, chini ya kifungu nambari 51 ya sheria ya umoja wa mataifa, inailazimu nchi “kuripoti mara moja” kwa baraza la usalama hatua yoyote ambayo imechukua katika haki ya kujilinda.

Awali Rais wa Marekani Donald Trump alisema Iran “inaonekana kurudi nyuma”baada ya kufyatua makombora dhidi ya kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq.

Bw.Trump, alisema kuwa hakuna raia wa Iraq au Marekani aliyeuawa katika shambulio hilo japo kambi hizo ziliharibiwa kidogo.

Kambi za kijeshi za Irbil na Al Asad zilishambuliwa mapema Jumatano alfajiri.

Iran ilisema ilichukua hatua hiyo kulipiza kisasi mauaji ya wiki iliyopita ya jenerali wake wa ngazi ya juu Qasem Soleimani.

Ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani ililenga msafara wake akiwa na maafisa wa wakuu wa kundi la waasi wanaoungwa mkono na Iran,mjini Baghdad katika hatua ambayo ilizorotesha uhusiano kati ya Iran na Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *