Man United waiadhibu tena PSG nyumbani

Man United leo wamevuna point tatu kutokea jiji la Paris Ufaransa baada ya kuwafunga wenyeji wa PSG katika ardhi ya kwao katika uwanja wa Parc de prince.

Kwenye mchezo huo licha ya Anthony Martial kujifunga na kuwafanya PSG wawe wamesawazisha dakika ya 55, Man United wameibuka kidedea kwa ushindi wa magoli 2-1.

Magoli ya Man United yakiwekwa nyavuni na nahodha wao wa mchezo Benjamin Fernandes dakika ya 27 kwa mkwaju wa penati na dakika ya 87 Marcus Rashford akafunga goli la ushindi kwa Man United ikiwa ni mchezo wao wa kwanza wa Kundi H.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *