MAMBO MAZITO BAADA YA LIGWARIDE SIMBA,WANNE WAFUTWA KAZI

IMEELEZWA kuwa Klabu ya Simba imewafuta kazi Mwarami Mohamed (Kocha wa magoli kipa) na Patrick Rweyemamu (Meneja wa timu ) kutokana na matokeo mabaya kwa mechi mbili Mfululizo
Simba imecheza mechi mbili mfululizo na kupoteza pointi sita ambapo ilianza kufungwa bao 1-0 mbele ya Tanzania Prisons Uwanja wa Nelson Mandela na ikachapwa tena bao 1-0 mbele ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Uhuru.

Kwenye mechi mbili ambazo zilikuwa zinahusisha timu za majeshi wenye mwendo wa kucheza ligwaride, Simba imeyeyusha pointi sita na kufungwa mabao mawili.

Pia inaelezwa kuwa wangine ambao wamefutwa kazi ni Ally Shatry ‘Bob Chico’ na Jacob ambao walikuwa kwenye kitengo cha Habari cha Klabu hiyo.

Wawili hao wamefutwa kazi kwa kile kinachosadikika kuwa karibu na CEO wa zamani Senzo Mazingiza ambae hivi sasa yupo Yanga.

Patrick Rweyemamu ambaye anatajwa kufutwa kazi hakuwa tayari kuzungumzia hilo pamoja na Katibu Mkuu wa Simba, Arnold Kasehembe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *