Makamu wa Rais Mgeni Rasmi CRDB Bank Marathon, Shilingi milioni 200 kukusanywa kusaidia upasuaji wa moyo kwa watoto 100

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amemshukuru Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika mbio za kwanza za hisani za “CRDB Bank Marathon” zinazolenga kuhamasisha uchangiaji wa shilingi milioni 200 kusaidia gharama za matibabu kwa watoto 100 wenye uhitaji wa upasuaji wa moyo. Nsekela ameeleza hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika makao makuu ya Benki ya CRDB, Azikiwe Jijini Dar es Salaam.

Nsekela alisema mbali na makamu wa Rais, viongozi mbalimbali ikiwamo Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete pamoja na Waziri wa Michezo, Harisson Mwakyembe wanatarajiwa kuungana na maelfu ya wakimbiaji kushiriki CRDB Bank Marathon tarehe 16 Agosti, 2020 katika viwanja vya “The Greens” Oysterbay, Dar es Salaam.

“Kauli mbiu ya mbiu yetu katika mbio hizi za hisani ni ‘Kasi Isambazayo Tabasamu’, ikihamasisha watu wengi zaidi kujitokeza kushiriki kuleta tumaini la maisha na kusambaza tabasamu kwa Watoto wenye magonjwa ya moyo,” aliongezea Nsekela huku akibainisha kuwa CRDB Bank Marathon mwaka huu inategemea kuwa na washiriki zaidi ya 4,000.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *