MAGUIRE AFUTA MAKOSA

HARRY Maguire, nahodha wa Manchester United dakika ya 23 aliweza kufuta makosa ya mchezaji mwenzake Luke Show aliyejifunga dakika ya 2 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Newcastle United.

Dakika 90 zilikamilika kwa United kusepa na pointi tatu baada ya kushinda kwa mabao 4-1 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa St.James Park.

Mabao mengine ya Manchester United yalifungwa na Bruno Fernandes dakika ya 86 na Aaron Wan-Bissaka dakika ya 90 na lile la nne lilipachikwa na Marcus Rashford dakika ya 90+6.

Sasa United chini ya Ole Gunner Solskjaer ina kibarua cha kumenyana na PSG Oktoba 20 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya utakaopigwa Uwanja wa Parc des Princes

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *