Magereza Masasi yaanza kutekeleza shughuli za kiuchumi, waanza kufuga samaki sato 800

JESHI la Magereza wilayani Masasi mkoani Mtwara limeanza uendeshaji wa shughuli za miradi mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo ufugaji wa samaki aina ya sato zaidi ya 800 kilimo cha Mahindi, Mpunga na mboga za majani.lengo ni kujitoleza kwa chakula na kifedha

Akiongea na waandishi wa habari jana ofisini kwake,mkuu wa gereza hilo, Gibson Mwakibibi alisema kufuatia agizo la serikali la kutaka kila gereza nchini kuanzisha shughuli za kiuchumi kwa ajili ya kujitosheleza kwa chakula pamoja na mapato ya ndani.

Alisema kutii agizo hilo uongozi wa gereza wilayani Masasi ulikaa na kutumia fursa walizonazo kwenye eneo lao kwa kubuni shughuli mbalimbali za kiuchumi  ikiwemo ufugaji wa samaki aina ya sato ambapo samaki hao watatumika kwa ajili ya biashara pamoja na chakula.

Mwakibibi alisema jeshi la magereza linamajukumu makuu matatu,jukumu la kwanza ni kuwapokea na kuwahifadhi wahalifu,jukumu la pili ni kuhakikisha usalama wa wahalifu wanapokuwa gerezeni na jukumu la mwisho ni kuwarekebisha wahalifu.

Alisema kutokana na majuku hayo gereza hilo kwa sasa limekuwa likiwaingiza wafungwa katika shughuli za uzalishaji mali kupitia miradi tofautitofauti kama vile kilimo, utengezaji wa sabani,vyuungu,ufugaji wa samaki,

“Katika shughuli zetu za uzalishaji mali kama vile kilimo cha mpunga msimu huu tumelima zaidi ya hekari mbili na tumepata gunia zaidi ya 35 za mpunga na hizi zitatusaidia kuwa chakula ndani ya gereza letu,”alisema Mwakibibi

Mkuu huyo wa gereza alieleza kuwa licha ya uanzishwaji huo wa mradi wa samaki lakini pia wameanza kulima bustani ya mboga za majani,ambapo miradi hiyo yote itasaidia kuongeza mapato ya ndani katika gereza hilo.

“Kwa sasa tuna mabwawa manne yenye samaki zaidi ya 800 lakini lengo letu kuwa na mabwawa zaidi ya 30 ya ufugaji wa samaki ili kuweza kuongeza tija zaidi katika ufugaji wa samaki,”alisema Mwakibibi

Alisema lengo kuu la kubuni miradi hiyo ya kilimo,ufugaji lakini pia utengenezaji wa vyiungu vinavyotengenezwa kwa kutumia saruji vya kuwekea mauwa majumbani,kunaiwa maji na kwamba kuona gereza hilo linaweza kujitegemea kiuchumi.

Mwakibibi alisema sehemu kubwa ya utekelezaji na ushiriki wa miradi hiyo ni kwamba imekuwa ikifanywa na wafungwa waliopo katika gereza hilo na kwamba hivi sasa kumekuwa na mabadiliko makubwa ya kiuchumi katika gereza hilo.

Alisema mradi mwingine ambao uko mbioni kuanza ni mardi wa utengezaji wa mifuko ya kisasa ambapo wazo hilo limeonyesha kuungwa mkono na wadau wengi wanaohitaji kununua mifuko hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *