Mafunzo ya Ualimu Nchini yaboreshwa……Taaluma ya ualimu ngazi ya cheti yafutwa

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania imeufuta mtaala wa ualimu wa ngazi ya cheti kwa elimu ya awali na msingi na kuanzisha wa Diploma ikwa ni hatua ya kuboresha elimu nchini
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Naibu Katibu Mkuu wizara hiyo, Dkt Ave Maria Semakafu, amesema hatua hiyo inakwenda sambamba na kufanyia kazi maoni ya wadau ambao wamekuwa wakiyatoa likiwemo kufuta mtaala huo.

Dk. Semakafu amesema, ulioboreshwa unatoa nafasi kwa mwalimu katika mwaka wa pili wa masomo kuchagua eneo la umahiri atakalobobea tofauti na mfumo wa zamani ambao haukuwa katika muktadha huo.

Amesema mtaala huo mpya utaanza kutumika katika mwaka wa masomo 2020/2012 na kwamba mwalimu yeyote mwenye cheti cha ualimu atakuwa na sifa ya kusomea Diploma ya Ualimu wa Elimu ya Awali au Msingi na vile vile atakapohitimu na kufaulu atakuwa na sifa ya kujiunga na chuo kikuu kupata shahada ya kwanza ya ualimu kwa elimu ya awali au msingi.

Aidha, amesema, walimu walioko tayari vyuoni wakisoma cheti ambao watamaliza mwaka 2021 hao ndiyo wa mwisho kudahiliwa.

Amesema, programu itakayofundishwa itakuwa ya miaka mitatu na kwamba masomo yatafundishwa kwa lugha mbili ambazo ni Kiingereza na Kiswahili kutokana na kuwepo kwa shule za English medium nchini.

Dkt Ave amesema, kwa walimu walioko kazini watakaopenda kujiendeleza wanaweza kusoma kwa masafa kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) kwa njia ya masafa, njia ambayo haita athiri utendaji na mwisho kufanya mitihani ili kupata Diploma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *