Maelfu ya Wairan wamuaga kamanda Soleimani

Kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ameongoza maelfu ya watu katika mji mkuu wa Iran, Tehran katika shughuli ya mazishi ya kamanda mwandamizi wa jeshi Qassem Soleimani.

Sauti ya Khamenei ilikwama kwa kipindi kifupi kutokana na machungu wakati kiongozi huyo alipokuwa akiongoza shughuli hiyo ya umma huku akishindwa kuzuia machozi.

Kulingana na televisheni ya umma nchini Iran, mamilioni ya raia wamejitokeza kwenye mitaa ya mji mkuu Tehran kutoa heshima zao za mwisho kwa kamanda huyo wa kikosi maalumu cha al-Qudskinachohusika na operesheni za kijeshi za nje.

Mkusanyiko huo unatajwa kuwa ni mkubwa zaidi wa mazishi tangu ule wa mwaka 1989 wa mazishi ya mwasisi wa taifa hilo la Kiislamu Ayatollah Ruhollah Khomenei, aliyeongoza mapinduzi yaliyoibua makwaruzano ya kisiasa na Marekani. Wengi wa wairan wanamuona Soleimani kama shujaa wa kitaifa na aliyechukuliwa kama mtu wa pili kwa mamlaka makubwa zaidi nchini humo baada ya Khamenei.

Umati katika mkusanyiko huo ulipaza sauti ukisema, “kifo kwa Marekani” na muombolezaji mmoja alibeba bango lililoandikwa “tuna haki ya kulipiza kisasi kikali”, matamshi ambayo awali yalitamkwa na viongozi wa kijeshi na kisiasa wa Iran.

Mwanaye wa kike Zeinab Soleimani amesema kwenye shughuli hiyo ya mazishi katika chuo kikuu cha Tehran kwamba, familia ya wanajeshi wa Marekani nazo zisubiri kushuhudia vifo vya wapendwa wao, alisema¬†“Familia ya wanajeshi wa Marekani kwenye eneo la Asia Kaskazini zimeshuhudia mateso ya Marekani katika vita vya Syria, Iraq, Lebanon, Afghanistan na Palestina na wao wasubiri kushuhudia vifo vya vizazi vyao”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *