Madiwani Waagiza Kuchukuliwa Hatua Kwa Wauguzi Waliosabisha Wakimama Kujifungilia Mapokezi

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge wamewaagiza Afisa Utumishi na Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) kuwachukua hatua Wauguzi wote walisababishia baadhi ya wakinamama kujifungulia mapokezi wakiwa wanasubiri huduma.

Azimio hilo limetolewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwenye  mkutano wa Baraza la Madiwani la Sikonge la kujadili na kupitia mapendekezo ya makisio ya mapato na matumizi ya mwaka 2020/21 baada ya baadhi ya Madiwani kulalamikia uzembe wa wauguzi ulisababisha baadhi ya wanawake kujifungua bila msaada wa Muunguzi.

Alisema ni vema wawaonyeshe hatua mbalimbali walizowachukulia Wauguzi wa Zahanati ya Kirumbi, Kisanga na Lembeli na watumishi walevi nyakati za kazi na Baraza la Madiwani lipatiwe taarifa.

Nzalalila alisema kama watashindwa kuwachukulia hatua itabidi Baraza limchukulie hatua Afisa Utumishi na Mganga mkuu wa Wilaya ya kushindwa kuwasimamia watumishi waliochini yao.

Awali Diwani wa kata ya Kipanga Upendo Mgombozi alisema mama mmoja mjamzito alilazimika kujifungulia mapokezi baada ya Muuguzi wa Zamu kudai hawezi kwenda kumsaidia kwa sababu ya hali aliyonayo kiafya.

Alisema mama huyo alijifungua mbele ya mume wake akiwa hana msaada wa Muuguzi yoyote na kuongeza kuwa angaweza hata kupoteza maisha kwa sababu ya kutokuwa na msaada wa mtaalamu.

Diwani huyo aliongeza kuwa hata alipomwita katika Kamati ya Kata kwa ajili ya kumuonya alishikiria msimamo wake kwamba asingeweza kumsaidia mama yule kwa sababu ya hali aliyokuwa nayo siku ile.

Akijibu hoja za Madiwani Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Dkt. Peter Songoro alisema baadhi ya wauguzi waliozembea na kusababisha baadhi ya  wanawake kujifungia wakiwa wanagonja huduma wameshapewa onyo na Muuguzi mwingine tuhuma zake zinaendelea kufanyiwa kazi na itakapokamilika watatoa taaifa ya hatua waliomchukulia.

Aliongeza kuwa Zahanati hazipaswi kufungwa bali zinatakiwa kufanyakazi saa 24 kila siku na kunakuwepo kwa mtumishi wa zamu kulingana na mpango kazi na ratiba ya zamu waliojipangia.

Aidha Dkt. Songoro aliwaomba Madiwani kuwahamasisha wananchi kushiriki katika ulinzi wa Zahanati katika maeneo yao.

Alisema kuwa Zahanati hizo zina miliki vifaa vya gharama kubwa na kunapokuwa hakuna ulinzi inasababisha hatari ya kupotea na wakati mwingine nyakati za usiku inasababisha maisha ya watu ambao wengine wanakaa mbali na Zahanati kuwa hatarini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *